Banki ya DCB yatoa mikopo ya bilioni 9.2 kwa wajasiriamali Ilala...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
BANKI ya DCB imesema toka
walivyoingia katika makubaliano ya kutoa mikopo na Manispaa ya Wilaya ya Ilala
mwaka 2014 kwa wanawake na vijana wajasiriamali tayari wameshaweza kutoa mikopo ya
takribani bilioni 9.2 kwa
vikundi 2978.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza
jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa(kulia) katika
banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya siku mbili ya
wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini
Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Godfrey
Ndalahwa alipokuwa akizungumza wakati wa
maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali yaliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya
Ilala Sophia Mjema kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
“Changamoto iliyopo kwa sasa ni uhitaji wa fedha kwani wanawake na
vijana wanaohitaji mikopo hiyo ni wengi katika manispaa na kuiomba Halmashauri
kuongeza fedha za mfuko huo ili kuwezesha benki kuwahudumia wajasiriamali wengi
zaidi.
“Tumelisikia ombi la
wajasiriamali la kutaka kuboreshwa kwa mikopo ikiwemo kuongezwa kwa kiasi cha
fedha pamoja na kukopesha vitendea kazi na vifaa kazi, sisi kama DCB benki
mteja wetu atakapohitaji vifaa atakuja kwetu na tutakaa chini na kuingia
makubaliano,”amesema na kuongeza Ndalahwa.
Katika
kuelekea kwenye
uchumi wa viwanda kama ilivyo adhima ya serikali ya awamu ya tano, Ndalahwa amewashauri wanawake
na vijana kuzingatia ubunifu na kutumia fursa za kiuchumi kupata mitaji na
kujiendeleza na kwamba benki
itandelea kutoa fursa za mitaji kwa wajasiriamali wa aina hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala
Sophia Mjema akizungumza baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya
wajasiriamali hao na kujionea namna wanavyofanya kazi zao amesema wameonesha
kuwa mikpo waloyokuwa wanaipata imekuwa na msaada mkubwa sana kwao na wameweza
kujiendeleza katika kukuza mitaji ya biashara zao na hata wengine waliweza
kuanzisha biashara nyingine na kujipatia faida.
“Wajasiriamali hawa
wameonekana kufikia malengo yaliyowekwa na rais John Magufuli kwa kuanzisha
viwanda, tumeona jinsi gani wameweza kutumia nafasi walizozipata hususani
katika mikopo waliyoipata na kujiendeleza zaidi,”amesema Mjema.
Benki ya DCB kwa
sasa hapa nchini inasifika kwa kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa
mikopo kwa vikundi mbalimbali vinavyojishugulisha na utengenezaji wa bidhaa za
vyakula, nguo, viatu na hata dawa za kusafishia ndani na vyooni.
Habari katika picha.
No comments:
Post a Comment