StarTimes yatangaza rasmi kurusha Kombe la Dunia Urusi 2018 Mubashara...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Star
Media (T) Ltd yenye chapa ya StarTimes leo imetangaza rasmi kurusha matangazo
ya Kombe la Dunia Urusi 2018 Mubashara kupitia king’amuzi chake.
StarTimes
imethibitisha kuonyesha michuano hiyo leo katika hafla fupi iliyofanyika
Terrace, Slipway Masaki na kushirikisha waandishi wa Habari pamoja na wadau
mbalimbali wa soka nchini.
Akiongea katika
uzinduzi huo Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bw. David Malisa alisema, “Mwaka huu
katika Kombe la Dunia la 21, StarTimes ni Mrushaji Rasmi wa michuano hiyo
ambayo itaanza tarehe 14 mwezi Juni hadi tarehe 15 Julai nchini Urusi. Mechi
zote 64 zitakazochezwa Urusi katika Kombe la Dunia zitarushwa moja kwa moja”.
Mbali na kurusha
tu michuano hiyo maarufu zaidi Duniani, StarTimes watarusha matangazo ya
michezo yote katika lugha ya Kiswahili, hii ni katika jitihada za kuienzi na
kuikuza lugha ya Kiswahili lugha ambayo ni maarufu zaidi katika ukanda huu wa
Afrika Mashariki.
“StarTimes tutarusha matangazo ya Kombe la Dunia, mechi zote
64 katika lugha ya Kiswahili pamoja na uchambuzi utakaoambatana
na mechi hizo, uchambuzi utakaofanywa na wachambuzi mahiri na tuliowazoea hapa
nchini”, aliongeza Bw. David.
Sambamba na
kuzindua Kombe la Dunia, StarTimes pia wametangaza Ofa kwa wapenzi wa Soka,
ambapo wateja watakaonunua King’amuzi ama Luninga zao za Kidigitali kati sasa
na Juni 30 watapatiwa Kifurushi cha Juu hadi Julai 31 Bure.
Chini ni matukio katika picha wakati wa uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment