Ummy: Serikali kutenga kila mwezi milioni 55 kwa Jiji la Tanga kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata elimu bora...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Tanga
WAZIRI wa
Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amesema serikali
kila mwezi imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 55 kwenye Jiji la Tanga
kwa ajili ya shule za msingi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila
kuwepo kwa vikwazo na hivyo kupata elimu bora.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy
Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya ufunguzi huo wa madarasa na makabidhiano
kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Aliyasema
hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi
Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwaka
mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje ya madarasa yaliyogharimu kiasi
cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani.
Ndani ya
kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule ya Msingi
Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri kwa
kiasi kikubwa taaluma.
Waziri Ummy
ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga alisema licha ya hivyo
lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 108 kwa
ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza
kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili kupitia sekta hiyo.
“Ndugu
zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo yamejengwa kwa
kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo lakini
pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali inaleta milioni 55 kila mwezi
kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi kushirikiana
nanyi”Alisema.
“Lakini pia
kadri tunavyoacha kwenda Marekani na Ulaya ndivyo fedha hizo zinasaidia
kutumika kwenye harakati za kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto
mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwapa watoto wetu elimu bora “Alisema.
Awali
akizungumza katika ufunguzi huo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga alisema ujenzi
wa majengo hayo yaliyotumia zaidi ya milooni 279 zilitokana na mapato ya ndani
ya halmashauri na kuongezewa na serikali.
Alisema
kutokana na kuwepo kwa hali hiyo wana mpongeza Rais Dkt John Magufuli kupitia
Wizara ya Elimu kuweka msukumo wao ambapo alihaidia kuzungumza na Waziri wa
Wizara hiyo kuweka mradi wa matokeo kwanza ndio wakapata na kupokea kiasi cha
milioni 136.6.
“Katika
suala hili naomba nikupongeze sana Mh Waziri Ummy kwa kulipigania Jiji la Tanga
ndani na nje kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto ambazo wamekuwa
wakikabiliana nazo hivyo nisema tutaendelea kushirikiana”Alisema.
Kwa upande
wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi aliishukuru serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa kuhakikisha ujenzi wa madarasa
hayo unakamilika kwa wakati ili wananfunzi waweze kuendelea na masomo.
“Tunaishukuru
Serikali kwa kusaidia ujenzi huu lakini Mh Waziri Ummy kwa msukumo mkubwa
uliouweka kwenye jambo hilo kwani shule waliokuwa wamehamia ya Mkwakwani
walikuwa na msongamano mkubwa na kusababisha kutokupata matokeo mazuri “Alisema
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha )
No comments:
Post a Comment