BREAKING NEWS!! 'KIMBEMBE CHA RUZUKU CUF' MAALIM AIBUKA KIDEDEA !!

Maalim Seif Sharrif Hamad
MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM MBELE YA MHESHIMIWA JAJI DYANSOBELA katika Shauri No. 28/2017 leo Tarehe 31/03/2017 IMETOA AMRI DHIDI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI JAJI FRANCIS MUTUNGI KUMZUIA KUTOTOA FEDHA ZA RUZUKU YA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) MPAKA SHAURI NAMBA 21/2017 DHIDI YA MSAJILI NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUHUSU KUTOA FEDHA ZA RUZUKU SHILINGI MILIONI 369 KWA NJIA ZA WIZI NA UDANGANYIFU LITAKAPOSIKILIZWA NA KUTOLEWA MAAMUZI.
Amri hiyo ya Mahakama Kuu imekuja baada ya Jopo la Mawakili wasomi wa Chama wanaoiwakilisha Bodi ya Wadhamini ya CUF (THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRON (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) Mhe. Juma Nassor, Mhe Daimu Halfani na Hashim Mziray kuwasilisha maombi hayo mbele ya Mahakama Kuu kuiomba Mahakama Kuu kutoa Amri hiyo kwa kuwa fedha zilizotolewa awali Milioni 369 hazijulikani zimetumika vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa Chama –CUF juu ya fedha hizo ikizingatiwa kuwa Lipumba alishavuliwa Uanachama. Wakili Msomi Juma Nassor aliyewasilisha maombi hayo aliweka mkazo na kusisitiza kuwa kwa mazingira yaliyopo ni vyema na Busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama Ruzuku kwa Chama Cha CUF kwa sasa ZIENDELEE KUBAKIA SERIKALINI. Aidha, Mawakili wasomi wameiomba Mahakama Kuu amri hiyo pia ifungamane na Kesi ya Msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya Msajili kumtambua Lipumba kwa Nafasi ya Uenyekiti iliyopo mbele ya Jaji Kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa Rufaa/maombi ya kufanyiwa Marejeo-REVISION mbele ya Mahakama ya Rufaa-Tanzania.

Mhe Jaji Dyansobela amekubaliana na Hoja zote hizo zilizowasilishwa kwa HATI YA DHARURA.

Imetolewa leo Tarehe 31/3/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search