MAKONDA NDANI YA KAMATI YA BUNGE
RC MAKONDA AWASILI DODOMA, KUHOJIWA NA KAMATI YA BUNGE LEO!

RC Makonda amepokelewa na Owen Mwandumbya ambapo aliitwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akitakiwa kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa inayodaiwa kuwa ni ya kulidharau na kulikashifu kwa wabunge.

Akitoa hoja katika mkutano wa bunge uliopita, Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara alisema kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.
==========================================================
==========================================================
Hapa chini ni picha za RC Makonda akihojiwa na kamati ya bunge leo mjini Dodoma.


No comments:
Post a Comment