OMG !! MESSI KIFUNGONI
FIFA imemfungia Lionel Messi!
Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA March 28 limetangaza taarifa ambazo haziwezi kuwa nzuri kwa mashabiki na wapenzi wa naodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye pia anaichezea FC Barcelona ya Hispania.

FIFA jana wametangaza kumfungia mechi nne Lionel Messi kufuatia kosa alilolitenda March 24 wakati wa mchezo dhidi ya Chile, Messi amefungiwa kutokana na utovu wa nidhamu wa kumtolea lugha isiyo ya kiungwana refa wa mchezo huo.

Adhabu hiyo ya Lionel Messi inaambatana na faini ya pound 8100, hivyo kufuatia adhabu hiyo Lionel Messi sasa ameanza kuitumikia kwa kukosa game ya jana dhidi Bolivia iliyomalizika kwa Argentina kupoteza kwa goli 2-0.
No comments:
Post a Comment