RC GAMBO AZINDUA HUDUMA YA TTCL 4G LTE JIJINI ARUSHA

Na Imma Msumba Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo Amezindua rasmi huduma ya TTCL 4G LTE Mkoani Arusha, Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu huyo wa Mkoa amesema,

"Nashukuru sana TTCL kwa kutuletea 4G LTE Mkoani kwangu maana Arusha ni Jiji la Kimataifa kutokana na kuwa kituo kikuu cha Sekta ya Utalii katika eneo hili la Afrika Mashariki. Pia Arusha ni Makao Makuu ya jumuia ya Afrika Mashariki, Soko la Kimataifa la Madini na vito vya thamani hasa Madini ya Tanzanite ambayo hayapatikani sehemu nyingine yoyote duniani, isipokuwa Mererani-Arusha-Tanzania. 
 
Aidha, Arusha ni kituo kikubwa cha Kitaaluma hapa nchini kikiwa na idadi kubwa ya shule na Taasisi za Elimu, Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda na Shughuli nyingine nyingi za Kitaifa na kimataifa." 

"Hata hivyo Arusha pia ni Jiji kubwa la kibiashara na kituo kikubwa cha shughuli za kiuchumi kati ya Tanzania na Nchi jirani hasa Kenya, Uganda, Sudan na nchi nyingine. Katika jamii hii ya Mkoa wa Arusha yapo makundi yenye idadi kubwa ya watu kama vile Wanafunzi, Wafanyakazi wa Sekta mbali mbali, Wafanyabiashara na Wakulima ambao wote hawa, wanahitaji sana Mawasiliano ya uhakika na yenye tozo nafuu katika kufanikisha shughuli zao. Natumia fursa hii kukuhakikishia kwamba, Arusha ni soko la uhakika la bidhaa na huduma za TTCL. Tunachohitaji ni huduma bora za uhakika." 

Kadhalika Rc Gambo alisisitiza kwamba yeye atakuwa mstari wa mbele kwa kutumia huduma ya hiyo "mimi binafsi na Watendaji wote walio chini yangu, kutumia huduma za TTCL ili kuhamasisha wengine kuiunga mkono Kampuni hii ambayo ni mali ya Wananchi kwa asilimia mia moja.nitalifikisha kwa wenzangu ili litengenezewe utaratibu mzuri wa utekelezaji. Ila mimi binafsi, tayari nimeshasajili namba yangu ya TTCL ambayo nitaanza kuitumia leo hii hapa mbele yenu wote mshuhudie." 
Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akihutubia kwenye uzinduzi huo wa TTCL 4G LTE .Pichani ni Kaimu Afisa mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Wazir Kindamba, Akizungumzia mipango na mikakati wa TTCL.

source: michuzi blog

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search