AFYA YA JAMII: MADHARA YA CHUMVI KWENYE MFUMO WA MKOJO WA BINADAMU

doc
Source: swahili times
Je umekuwa ukisumbuliwa na hali ya kupatwa na mkojo mara kwa mara wakati wa usiku, jambo ambalo huukatiza usingizi wako?
Zifahamu sababu zinazoweza kuwa ndio chanzo cha hali hiyo kwako na namna ya kuondokana nayo.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na madaktari wa Japan umebaini kuwa chanzo kikubwa cha kukojoa sana wakati wa usiku husababishwa na ulaji wa chumvi kwa kiwango kikubwa.
Katika ripori iliyotolewa na CNN, madaktari kutoka Chuo kikuu cha Nagasaki walisema kuwa hali ya kuhisi mkojo kwa wingi wakati wa usiku (nocturia) inaweza kuhusishwa na kiwango cha chumvi kilichopo kwenye chakula.
KN
Katika utafiti ulioshirikisha watu zaidi ya 300, ilithibitika kuwa watu wanaotumia kiwango kidogo cha chumvi kabla ya kulala hupatwa na mkojo mara chache sana wakati wa usiku.
Japokuwa mtafiti anayejulikana kama Dr Matsuo Tomohiro, alisema kuwa kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku huwapata zaidi watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60. Hali hii inaweza kupunguzwa kama watazingatia kiwango cha chumvi.
Image result for a man urinating
Hata hivyo, matabibu wameeleza kuwa kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku kunaweza kusababishwa na unywaji wa maji mengi kabla ya kulala.
Wakati huo huo, wataalamu hao wa matibabu wametoa maoni kwamba kupatwa na mkojo mara nyingi wakati wa usiku inaweza kuwa ni dalili ya matatizo ya kiafya kama vile kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine mengi.
Hivyo ni vyema kuijua afya yako kila mara ili kuepukana na matatizo yanayoweza kukuletea madhara katika maisha yako.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search