MWANASIASA MSOMI ZITTO KABWE AMEYASEMA HAYA JUU YA NAMNA YA KUWAPATA WAGOMBEA WA BUNGE LA EALA KUTOKA KUNDI LA VYAMA VYA UPINZANI!

Moja ya habari iliyochukua headlines kwenye magazeti ya leo ni pamoja na kuhusu Zitto Kabwe na CHADEMA kudaiwa kutifuana sababu ikiwa ni uchaguzi wa ubunge wa Afrika Mashariki ‘EALA’. Aidha mijadala mikali imeendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uchaguzi huo kundi la vyama vya Upinzani.
Sasa kupitia ukurasa wake wa Facebook Kiongozi wa ACT Wazalendo ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameyaandika haya…..
ACT Wazalendo kama chama chenye uwakilishi Bungeni kina haki ya kuweka wagombea na tumeshamteua Prof. Kitila Mkumbo katika nafasi 1 kati ya nafasi 3 za Vyama vya Upinzani.
Ninaamini kuwa nafasi 1 hii kuchukuliwa na Mtanzania wa kaliba ya Prof. Kitila Mkumbo haiwezi kuwa ndio hatma ya Upinzani nchini. Eti nafasi moja EALA inayoombwa na ACT Wazalendo kati ya nafasi 3 zilizopo iwe chanzo cha kuvunja Umoja wetu kwenye masuala makubwa ya nchi? We have a war to fight, EALA is just one of the battles. Haiwezi kuwa ndio hatma ya vita kubwa.
No comments:
Post a Comment