BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI KENYA DKT. PINDI HAZARA CHANA ARIPOTI KWENYE KITUO CHAKE CHA KAZI

Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya, Mheshimiwa Dkt. Pindi Hazara Chana ameripoti kwenye kituo chake cha kazi jijini Nairobi na kulakiwa na wafanyakazi wa kituo hicho.
Balozi Chana amekutana na wafanyakazi wa kutoka nyumbani na wale walioajiriwa hapa Kenya. Balozi ameelezea kituo cha Nairobi kama moja ya vituo vyenye shughuli nyingi na vinavyosifiwa kwa utendaji mzuri licha ya mazingira magumu ya kazi. Amewaahidi wafanyakazi kuwa atakuwa kiongozi wa kujichanganya kwani anaamini katika uwazi, umoja na mshikamano kazini.
"Nitajichanganya sana na ninyi kwa sababu nimetumwa kuwatumikia watu. Sera yangu ya kazi ni uwazi, upendo na mshikamano. Tufanye kazi kama familia moja," alisema.
Balozi Chana amesema Kenya ni jirani mwema wa Tanzania na nchi hizo zina historia ndefu ya undugu na ushirikiano, hivyo kazi yake ni kuhakikisha ushirikiano huo unaimarishwa na kudumishwa.
Source: Michuzi blog 
 Balozi Chana akikaribishwa kwenye ofisi za Ubalozi na Mwambata wa Utawala, Bi Aneth Mmari
 Balozi akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi. Wa kwanza kulia ni Konseli Mkuu wa Tanzania Mombasa, Mheshimiwa Khalifan Shehe Saleh
 Balozi Chana akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi waliojipanga kumlaki.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search