BREAKING NEWS!! KUNA UVAMIZI MAENEO UA MBURAHATI UNAKOFANYIKA MKUNATO WA CUF

























#UVAMIZI : Inaripotiwa kwamba kuna uvamizi umefanyika katika hoteli ya Vinna  iliyopo Mburahati -  Dar es Salaam ambapo kulikuwa na 'press conference ' ya baadhi ya wanachama wa Chama Cha Wananchi ( #CUF ).

Wanachama hao ambao wanamuunga Mkono Maalim Seif, waliitisha mkutano na waandishi wa habari kueleza juu ya ujio wa Maalim Seif na mambo mengine yanayowahusu lakini mkutano huo ulivamiwa na watu wenye mapanga na mmoja mwenye bastola.

Inasemekana kwamba watu waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif ni kutoka upande unaomuunga mkono Prof Lipumba.

Walipovamia mkutano huo waliwashambulia wazungumzaji na baadhi ya waandishi habari waliokuwepo ndani ya chumba cha Mkutano. Pia waliwazuia kutoka nje hadi pale wananchi wa eneo hilo walipofahamu kinachoendelea na kuanza kupiga kelele.
Wavamizi walikimbia lakini mtu mmoja aliyeshukiwa kuwa mmoja ( anayeonekana pichani ) wao amekamatwa na kushambuliwa na Wananchi wa eneo hilo.
#UVAMIZI : Inaripotiwa kwamba kuna uvamizi umefanyika katika hoteli ya Vinna  iliyopo Mburahati -  Dar es Salaam ambapo kulikuwa na 'press conference ' ya baadhi ya wanachama wa Chama Cha Wananchi ( #CUF ).

Source: clouds media

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search