BREAKING: TRA WAKAMATA BASI LA SERENGETI BOYS LIKIELEKEA KWA MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU

2DAR 

ES SALAAM: Mamlaka  ya Mapato Tanzania (TRA) wamelikamata basi la timu ya Taifa vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) walilokuwa wakilitumia kwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu kwa ajili ya chakula cha usiku.
TRA wamekamata basi hilo kupitia kwa Kampuni ya Udalali ya YONO ambapo basi hilo linamilikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Basi hilo ni la timu ya taifa ya Tanzania lakini kwa sasa linatumiwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
Gari limechukuliwa katika Hotel ya Urban Rose likiwa linawasubiri wachezaji wa Serengeti Boys liwapeleke kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu.
Sababu ya kukamatwa kwa basi hilo ni deni la kodi ya mapato ambayo TFF inadaiwa.
Source: swahilitimes.com

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search