MAONI YA WATU MBALIMBALI KUHUSU RAIS MAGUFULI KUMTEUA PROF. KITILA MKUMBO

Rais Dkt Magufuli ameteua viongozi mbalimbali kuwa makatibu wakuu lakini miongoni mwao, mmoja tu ndiye aliyezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.
Rais Magufuli amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo ambaye ni mwanachama wa ACT- Wazalendo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Prof. Kitila Alexander Mkumbo ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.
Sababu kuu mbili zilizosababisha watu kujadili zaidi uteuzi huu ni, moja, kauli ambayo Prof. Mkumbo aliyoitoa kipindi cha nyuma kuhusu wahadhiri kuteuliwa kutoka vyuoni ambapo alisema, “Huu utaratibu wa kuwateua wasomi tu ambao ni walimu na wanataaluma kutoka vyuo vikuu hasa Chuo kikuu cha Dar es salaam si mzuri maana rais haoneshi kuwaandaa wengine kuchukua nafasi zao, tuachwe wasomi tufanye kazi za kitafiti na kitaaluma.”
Wengi wamehoji je atasimamia kauli yake? Lakini pili ni kauli ya Rais Magufuli aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara akiwa Unguja kuwa kwenye serikali yake hatoteua mtu kutoka chama cha upinzani.
Source:Swahili times
No comments:
Post a Comment