BUNGE 'LALIPUKA' JK AKIMSINDIKIZA MAMA SALMA KULA KIAPO... ASEMA NI ZAMU YANGU KUMUUNGA MKONO !!


Mkutano wa saba wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo Dodoma kwa kushuhudia tukio la kuapishwa kwa Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano Tanzania kwaa mara ya kwanza.
Lengo kuu la Mkutano huu ni kupitisha bajeti ya Serikali itakayowasilishwa bungeni June 15 mwaka huu.

Pichani: Mama salma akisindikizwa na wabunge wenzake wakati akiingingia ukumbini leo.

Miongoni mwa wageni waliotambulishwa leo bungeni ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo ukumbi mzima ulilipuka kwa vifijo na nderemo za 'tumekumic - tumekumic' tumekuekea tukio hili bonyeza kiunganishi hapa chini...


akiongea baada ya Mama Salma kula kiapo, Rais huyo mstaafu alisema sasa ni zamu yake kumuunga mkono mkewe wakati akitekeleza majukumu yake hayo mapya.

'Nimeshuhudia kiapo cha Mke wangu Mhe. Salma Rashid Kikwete kuwa Mbunge wa Kuteuliwa Bungeni Dodoma.Ni zamu yangu kumuunga mkono

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search