BREAKING NEWS !! BEI UKOMO YA MAFUTA YA PETROL YASHUKA..



Picha: moja wapo ya vituo vya mafuta ambavyo kuanzia kesho wananchi wanatarajiwa kumiminika kwa wingi kujipatia huduma kufuatia EWURA kushusha bei kikomo kuanzia.

Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura)imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoaanza kutumika kuanzia kesho.

Meneja wa Mawasiliano wa Ewura,  Titus Kaguo aliwaambia wanahabari kuwa petroli imeshuka kwa Sh 3 itakuwa inauzwa Sh 2057 kutoka 2060, dizeli imepanda kwa Sh 12, kutoka Sh 1913 hadi 1925 na mafuta ya taa ni Sh 1958 kutoka 1952.

Kiguo alisema mabadiliko hayo ya bei yametokana na  bei za mafuta katika soko la dunia kubadilika sanjari na mfuko wa bei na gharama za usafirishaji.

Source: mwandishi maalum - Tanzania Mpya Matukio

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search