KIMATAIFA: 'FIGISU FIGISU' ZA UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA; WAPINZANIA WAJIPANGA KIVYAO..

Maafisa wakisimamia wapiga kura katika chaguzi zilizopita
Hisia tofuati zimeibuka nchini Kenya kufuatia kauli iliyotolewa hivi karibuni na upinzani National Supper Alliance (NASA) kuhusu mpango wa kuwa na kituo cha kuhesabia kura wakati wa uchaguzi mkuu Agosti, kitakacho endesha shughuli sambamba na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Vyombo vya habari Kenya, vinaripoti kuwa tume ya IEBC inasema mipango hiyo ya NASA itakwenda kinyume na sheria nchini.
Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga amekuwa akisisitiza tuhuma kwamba uchaguzi wa mwisho mnamo 2013, ulikumbwa na udanganyifu.
Mwenyekiti wa (IEBC) Wafula Chebukati
Katika mkutano wa kisiasa hivi karibuni, bwana Odinga alinukuliwa na vyombo vya habari nchini akisema, 'Tunachotaka ni kuwa, katika kila kituo cha kuhesabu kura tutakuwa na vijana 50, watawasiliana na sisi kupitia video na kutujuza ni nani aliyepiga kura na ni nani ambaye hakupiga".

Ina maana gani kisheria?

Mratibu wa kitaifa kutoka jukwaa la uangalizi wa uchaguzi ELOG Mulle Musau anasema, ni kinyume cha sheria kuidhinisha vituo vya kupiga, kuhesabu na kutangaza kura wakati wa uchaguzi, kando na vituo rasmi vya tume ya uchaguzi nchini IEBC.
Kwa upande wa upinzani, inaweza kuruhusiwa kuwa na vituo maalum vinavyostahili kuwa vya kuendesha shughuli za chama hicho, wakati wa uchaguzi mkuu.
Musau anaongeza kuwa ili mradi chama hicho kitatumia matokeo ya mwisho yatakayo kuwa yanamiminika katika vituo mbali mbali vya tume rasmi ya uchaguzi Kenya IEBC, basi hakuna makosa.
Wafuasi wa Raila baada ya mahakama Kenya mnamo 2013 kuidhinisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta
'Ni desturi ya vyama vya kisiasa nchini kufanya hivyo na ni jambo ambalo limekuwa likifanyika hata kwa waangalizi wa uchaguzi na vyombo vya habari katika kufuatilia matokeo'.
Hofu iliopo ni iwapo upinzani utaamua kutangaza matokeo yake kabla ya matokeo rasmi ya IEBC, jambo linalohofiwa kwamba huenda likazusha mzozo wa kisiasa nchini.
SOURCE: BBC SWAHILI

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search