KAMATI YA FORODHA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YATOA RIPOTI YA MAENDELEO KATIKA UTEKELEZWAJI WA MALENGO YA UMOJA

Kaimu Kamishna Kitengo cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato hapa Nchini(TRA), Qamdiyay Akonaay (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo katika mkutano huo uliomalizika leo Aprili 27,2017.

Washriki wa mkutano huo wakiendelea kufuatilia kilichokuwa kikiendelea.

Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea.

Kamishna wa Forodha Nchini Uganda, Dickson c. (katikati) Kateshumbwa akizungumza jambo katika mkutano huo.
Picha zote na Philemon Solomon
Akisoma taarifa hiyo mbele ya vyombo vya habari Kamishna wa Forodha Nchini Uganda, Dickson c. Kateshumbwa amesema kuwa mkutano wa Umoja wa Forodha kwa nchi zilizo kwenye uanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki hufanyika kwa zamu nchi zote za uanachama. Ambapo kwa mwaka huu mkutano huo umefanyika hapa nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa kila mwaka mkutano huo hufanyika katika ngazi tatu, ambazo ni ngazi zinayohusisha wataalamu wa masuala ya forodha ambao hutoka katika mamlaka za mapato za kila nchi wanachama, na ngazi ya pili ni makamishna wote wa forodha walio katika nchi wanachama huku ngazi ya tatu ni makamishana wote wakuu ambao jukumu lao huwa ni katika kuidhinisha mipango na mikakati pamoja na kutoa maelekezo na maagizo kwa ajili ya kuhakikisha mipango na mikakati inatekelezwa.
Alifafanua kuwa lengo la jumuiya ya Afrika mashariki ni kuhakikisha inatekeleza miradi mbali mbali ya forodha yenye lengo la kurahisisha na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara na wananchi wote wanapata faida kwa ujumla.
Naye Kaimu Kamishna Kitengo cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato hapa Nchini(TRA), Qamdiyay Akonaay ametaja miradi iliyo katika mfumo huo wa forodha kwamba ni pamoja na himaya moja ya forodha, muunganiko wa huduma za kiforodha, kituo kimoja cha huduma Mpakani na wafanyabiashara wenye kuidhinishwa huweza kupata huduma maalumu.
Mkutano huo ulianza Aprili 21 mwaka huu na umemalizika leo Aprili 27 ambapo maazimio mbalimbali juu ya mkutano huo yamejadiliwa na miongoni mwa hayo ni, mpango wa kuwa na himaya moja ya forodha, muunganiko wa huduma za kiforodha na mapitio ya viwango vya ushuru na kanuni za uasili wa bidhaa.
No comments:
Post a Comment