"KITILA CAN GO..."ZITTO AONGELEA MASLAHI YA NCHI YETU.. ASEMA NI ISHARA TOSHA KUWA HATA NDANI YA UPIZANI KUNA UZALENDO NA UPEO WA KULITUMIKIA TAIFA KATIKA NAFASI MBALI MBALI.
#BREAKING Kiongozi wa ACT @ZittoKabwe apokea barua ya kujiuzulu ya @kitilam baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa Wizara #MillardAyoUPDATES
Akiongea na waandishi wa habari mchana huu mjini Dodoma, Zitto amesema wamempa baraka zote Dkt. Kutumikia nafasi hiyo mpya kama Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kama chama kitampa ushirikiano unaohitajika katika kufanikisha majukumu yake.
Amesema uteuzi huo ni ishara tosha ya Uzalenda na dalili kwamba hata ndani ya upinzania kuna Watanzania wenye uwezo wa kulitumikia Taifa.
Zitto: Kitila ni mtumishi wa umma kwa sababu ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa hio nafasi aliyopata ni kupanda cheo tu ndani ya utumishi wa umma, ni sawa kama angeteuliwa kuwa Vice Chancellor wa chuo kikuu.
Kwa nafasi ya katibu mkuu, Ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa mshauri wa chama, nafasi ambayo inamfanya ahudhurie vikao vyote vya chama kuanzia ngazi ya chini mpaka kamati kuu na kamati ya uongozi.
Prof. Kitila ameandika barua ya kujiuzulu ushauri wa chama, nimeipokea barua yake na nimemkubalia kujiuzulu kwake kuanzia Leo. Chama kinamshukuru sana mheshimiwa Kitila kwa wakati wote alichokitumikia chama toka tulipoanza chama hiki alipokuwa mshauri wa chama.
Kaulimbiu yote siku zote ni taifa kwanza, leo na kesho hivyo tunamtakia kila laheri ndugu Kitila katika nafasi hii mpya, wizara ni kubwa na muhimu katika nchi yetu.
Zitto amesema hawawezi kuwanyima watanzania mtu mwenye weledi kwa kuweka maslahi ya chama mbele, amedai Kitila hawezi kukataa uteuzi kwa sababu yuko kwenye utumishi wa umma na hiyo ni nafasi tu kama ya kupanda cheo.
Zitto amesema hio inaonyesha kuna watu nje ya chama cha mapinduzi wanaoweza licha ya Rais Magufuli kujua anatoka upinzani.
anasema walifanya mashauriano kama chama ikiwemo Kitila Mkumbo, chama kimepokea uteuzi wa Kitila kuwa katibu mkuu. Uteuzi unaonyesha upinzani kuna watu wenye uwezo, weledi na uzalendo wa kuweza kutumika katika utumishi wa Umma.
Zitto: Kitila ni mtumishi wa umma kwa sababu ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa hio nafasi aliyopata ni kupanda cheo tu ndani ya utumishi wa umma, ni sawa kama angeteuliwa kuwa Vice Chancellor wa chuo kikuu.
Kwa nafasi ya katibu mkuu, Ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa mshauri wa chama, nafasi ambayo inamfanya ahudhurie vikao vyote vya chama kuanzia ngazi ya chini mpaka kamati kuu na kamati ya uongozi.
Prof. Kitila ameandika barua ya kujiuzulu ushauri wa chama, nimeipokea barua yake na nimemkubalia kujiuzulu kwake kuanzia Leo. Chama kinamshukuru sana mheshimiwa Kitila kwa wakati wote alichokitumikia chama toka tulipoanza chama hiki alipokuwa mshauri wa chama.
Kaulimbiu yote siku zote ni taifa kwanza, leo na kesho hivyo tunamtakia kila laheri ndugu Kitila katika nafasi hii mpya, wizara ni kubwa na muhimu katika nchi yetu.
Zitto amesema hawawezi kuwanyima watanzania mtu mwenye weledi kwa kuweka maslahi ya chama mbele, amedai Kitila hawezi kukataa uteuzi kwa sababu yuko kwenye utumishi wa umma na hiyo ni nafasi tu kama ya kupanda cheo.
Zitto amesema hio inaonyesha kuna watu nje ya chama cha mapinduzi wanaoweza licha ya Rais Magufuli kujua anatoka upinzani.
No comments:
Post a Comment