KUTOWEKA KWA MSANII ROMA NA WENZAKE; WAZIRI MWIGULU ATOA MAAGIZO !!

H22A1910

    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa ameshtushwa na kutoonekana kwa mwanamuziki Roma Mkatoliki pamoja na wenzake waliokamatwa wakiwa katika Studio za Tongwe Records.
Akiwa kama Waziri mwenye dhamana ameagiza Jeshi la Polisi kufuatilia kujua undani wa tukio hili, hatma ya wasanii hao na pia watoe taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa tukio leo.
Waziri nchemba aliyasema hayo jana kupitia ukurasa wake w a Instagram ambapo aliandika, Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa ,zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma"
Source: swahilitimes.com

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search