MANENO YA MBUNGE PETER LIJUALIKALI (CHADEMA) BAADA YA KUTOKA GEREZANI

Mbunge wa Kilombero mkoani Morogoro, Peter Ambrose Lijualikali amesema kuwa ilikuwa ni fahari kwake kukaa gerezani kwa takribani miezi miwili na nusu sababu ya kutetea haki za wanyonge.
Ni heshima kubwa, nimefungwa kwa sababu ya kukataa uchakachuaji. Walinifanyia vurugu halafu baadae wakanigeuzi kesi wakisema mimi ndiye niliyefanya vurugu.
Mbunge huyo wa CHADEMA aliyesema hayo baada ya kuachiwa huru katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam kufuatia Mahakama Kuu kutengua hukumu ya kifungo cha miezi sita aliyokuwa amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero.
Mbunge huyo ailisema viongozi wengi wa vyama vya upinzani nchini wamekuwa wakionewa bila kujali nyadhifa na heshima zao kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kubambikiwa kesi kama ilivyokuwa kwake yeye. Alihoji pia, kama Mbunge anaweza kubambikiwa kesi na kufungwa ili matakwa ya baadhi ya watu yatimie, itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida?
Mahakama Kuu iliamuru kuachiliwa kwa mbunge huyo aliyefungwa kwa kosa la kufanya vurugu kwenye uchaguzi baada ya kubaini mapungufu katika hati ya mashtaka ya kiongozi huyo..
source: swahili times 


Peter-Ambrose-Lijualikali

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search