MATUKIO KIMATAIFA: MBEKI 'AELEMEA' UPINZANI

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki anawataka wabunge wa chama cha ANC kutenda yatakayowafaa raia na sio kile kitakachofaidi chama, wakati wa kujadili mswada wa kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma, wiki ijayo.

Wito wa Mbeki huenda ukawakera wanaomuunga mkono Zuma ambao wameapa kuupinga mswada huo vikali bungeni, kulingana na tovuti ya IOL.
Upinzani unadai kuwa Zuma ni mfisadi na kuwa alimfuta kazi Pravin Gordhan kama waziri wa fedha, licha ya kuwa Gordhan aliheshimika sana.
Wanasema nia ya Zuma ilikuwa kuchukua usukani katika wizara ya fedha.
Zuma anakanusha madai ya ufisadi akisema kuwa yeye kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na ni kwa manufaa ya raia 
Kulingana na tovuti hiyo, Mbeki alisema kuwa wabunge wanafaa kuwa sauti ya wananchi na wala sio sauti ya vyama vya kisiasa.
Anasema huu ni wakati wa Afrika Kusini kujua ukweli kuhusu uhusiano wa kikatiba kati ya wananchi na viongozi wao wa kisiasa.
Mbeki ni mwanachama wa ANC ambaye alijiuzulu kama rais baada ya kupoteza imani kwa chama hicho kinachoongozwa na Zuma, mwaka wa 2008.

Source: bbc swahili

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search