MATUKIO PICHANI: BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUA MBIO ZA MWENGE KITAIFA; AHIMIZA USHIRIKIANO WA WANANCHI NA SERIKALI

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga (kulia) akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alipowasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017.

Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mwenye miwani) akiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

: Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akitoa salamu toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo ya mwenge wa uhuru 2017 kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu za Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kukabidhiwa mwenge huo kuukimbiza kwa siku 195 katika mikoa 31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akimpa mkono wa baraka kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour kabla ya kumkabidhi mwenge huo kuukimbiza katika mikoa 31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto) akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour (kushoto) akimhaidi mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (kulia) kuulinda na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote 195 Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa mwenge huo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri 195 Tanzania bara na Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

Watumbuizaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari wakitoa burudani wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi
No comments:
Post a Comment