MWAKIEMBE AKUTANA NA VIONGOZI WA SIMBA MJINI DODOMA



Uongozi wa timu ya Simba ukiongozwa na Rais wa timu hiyo, Evans Aveva leo umekutana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe katika Ofisi zake Mjini Dodoma.
Uongozi wa Simba umeitikia wito wa Dkt. Mwakyembe wa kukutana naye ili waweze kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa Miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko na maendeleo ya mpira na uendeshaji wa timu hapa nchini.
Aidha, Katika hatua nyingine Mwakyembe  amepokea maoni ya Uongozi wa Simba na kushauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu.
Hata hivyo, Kikao hicho pia kilihudhuriwa  na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof. Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Omary, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja, na Msajili wa Vilabu na Vyama hapa nchini

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search