FA CUP: YANGA NA PRISONS KATIKA 'MIZANIA KALI'
Na: Samuel Samuel:
Mgomo , uchumi mbovu lakini bado kocha anawajenga kisaikolojia wachezaji wanamuelewa na kuonesha kiwango kizuri na kushinda mechi muhimu . Mechi inayowapeleka nusu fainali ya ASFC . Wamerudi vipande vipande toka Algeria na kupata muda wa kufanya mazoezi usiozidi saa 72 lakini leo uwanjani unaiona timu inayocheza katika misingi bora ya kiufundi, kimbinu na saikolojia nzuri ya kusaka ushindi.
Si kwamba ni shabiki sana wa Lwandamina kiasi kwamba nisione mapungufu yake , lakini unatizama yupo katika wakati gani na timu na kile anachokipata baada ya dakika tisini na jinsi gani timu inacheza ( Chemistry, rhythm and tempo )
Mathalani mfano mdogo i.e si mwalimu mwenye kinyongo na mchezaji . Ni mwalimu ambaye anajali masilahi ya timu kwanza . Mnakumbuka varangati la Bossou ?! Mwalimu mwingine mpaka leo si angekuwa benchi ? Chirwa na hekaya za Algeria leo imekuwaje ?
Sasa ukinielewa hapo ndipo unakuja kupata picha angeikuta ile Yanga ya kukaa kambini Uturuki wiki mbili ingekuwaje . ?!
Lakini sio GL tu , pia sifa hizi zinaenda pia kwa msaidizi wake Juma Mwambusi .
Waalimu wa mpira wanatofautiana sana kwa packages walizonazo vichwani mwao kutokana na taaluma waliyopata .
Katika benchi la ufundi kuna vitu viwili muhimu sana ; FOOTBALL COACHING AND FOOTBALL MANAGEMENT. Waalimu wana ' coaching ' package pekee na hawana ' management ' hivyo ni rahisi pia kuanguka katika mipango yao pale klabu inapopitia matatizo makubwa kifedha na kiutawala .
Mwambusi pekee mtizame akiwa na ile Mbeya City iliyopanda ligi msimu wa 2013-14 . Utamuona mjenzi wa morali , ari na nguvu ya kupambana kusaka alama tatu katika mazingira yoyote yale . Ukija kwa GL toka akiwa Zesco anasifika katika kuvumilia shida na ku ' maintain ' nidhamu ya timu katika kupambana pia si muongeaji sana na vyombo vya habari kitu ambacho hutunza siri na heshima yake hata kama yupo katika maji ya shingo . Ana kipawa cha kumfanya mchezaji yoyote katika timu kujiona ni msumari muhimu wa mwisho katika nguzo ( egemeo )
TUHESHIMU TAALUMA ZA WATU ILI TUPATE SOMO SAHIHI JINSI GANI YA KULIPELEKA MBELE SOKA LETU .

No comments:
Post a Comment