NAY WA MITEGO - LIVE COVERAGE XXL YA CLOUDS FM
Mwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego amesema kuwa usalama wa maisha yake kwa sasa ni mdogo sana kutokana na baadhi ya watu kumtisha kutaka kumuua.

Aidha, Nay amesema kuwa licha ya kuwa anakumbana na vitisho vyote hivyo hawezi kuhama nchi wala kukimbilia popote na kwamba ataifia hapa hapa nchini;
“Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa, Wana panga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakua na chakuongea,” aliandika Nay.
Aliandika pia, “Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod
.”

No comments:
Post a Comment