KIMATAIFA: POLISI WA DORIA NCHINI KENYA WAMEKUWA WAKITUMIA RISASI KUUA MIFUGO YA JAMII ZA WAFUGAJI


Ripoti ya kutoa kituo cha televisheni cha NTV cha nchini Kenya zinasema kuwa maafisa wa usalama waliotumwa eneo la Laikipia kufuatia uvamizi ulitokea katika mashamba ya kibinafsi na mahoteli uliofanya na wafugaji, wamekuwa wakiwaua kwa kuwapiga risasi mifugo wanaomilikiwa na jamii za wafugaji Awali mamlaka zilikana madai kuwa polisi wamekuwa wakiwaua mifugo kulipiza uvamizi wa wafugaji hao. Ukame unaoendelea kushuhudiwa unaripotiwa kuwalazimu wafugaji kutafuta malisho kwenye mashamba ya kibinafsi, lakini baadhi yao wameripotiwa kupora na kuchoma moto hoteli za kibinafsi.



Mmoja wa wafugaji aliyehojiwa alisema kuwa polisi waliwaua mifugo wake kwa kuwapiga risasi.
Source: Bbc swahili.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search