SALUM MKEMI NAE YAMKUTA YA HAJI MANARA, BODI YA LIGI TANZANIA YAMSHITAKI KWENYE KAMATI YA NIDHAMU
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amefunguliwa na mashitaka na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB).
TPLB inamtuhumu Mkemi kutoa matamshi ya kuudhi dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mkemi anadaiwa kuwadhalilisha viongozi wa TFF kwa madai kwamba alidai amefikisha suala la viongozi wa kamati ya Saa 72 Takukuru.
Hata hivyo, TFF na bodi ya ligi ziliendelea kukaa kimya bila ya kuchukua hatua hadi wadau walipoanza kulalamika kuhusiana na kufungiwa kwa Msemaji wa Simba, Haji Manara.
No comments:
Post a Comment