NEWS ALERT ! MTUMISHI WA KAMBI YA WATALII AVAMIWA NA KUJERUHIWA VIBAYA NA SIMBA(MNYAMA)
Mtumishi wa kambi ya watalii Maramboy Tented Kilopa Loyani(46) amevamiwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo kunyofolewa sikio lake la upande wa kushoto.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Idara ya mawasiliano ya Hifadhi ya Taifa (Tanapa) ilibainisha kuwa baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambayo ni jirani na kambi hiyo ndiyo walishiriki kikamilifu kumsaidia majeruhi huyo kumpeleka Hospitali ya Kilimanjaro Christian Center (KCMC) kwa matibabu ambapo amelazwa.
"Shirika la Hifadhi la Taifa linaweka kumbukumbu sawa ili kuondoa mkanganyiko mlinzi huyo akiwa kazini alijerihiwa na simba siku ya Jumamosi tarehe 22.4.2017 saa 9 usiku,"alisema Paschal Shelutete Meneja uhusiano wa Tanapa.
Shelutete alisema ameyaeleza hayo ili kuondoa taarifa tofauti potofu zilizosambazwa awali kwenye mitandao ya jamii zikidai kuwa majeruhi huyo ni Mwalimu alijeruhiwa akitoka kula chakula cha usiku kwenye mbuga ya Serengeti huku nyingine zikieleza kuwa ni Askari wa wanyamapori katika Hifadhi ya Tarangire.
No comments:
Post a Comment