Mjue kocha mpya wa Simba ...soma habari kamili na matukio 360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam


KLABU ya Simba imemtangaza rasmi, Mfaransa Pierre Lechantre kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo


Kocha Mkuu mpya wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre.

Mkuu wa habari Simba, Haji Maabara amesema kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Afrika 2000.

Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 ba pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi.

"Na leo jioni kocha Lechantre anaishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa," amesema Manara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search