STANDARD GAUGE YANOGA: JPM KUWEKA JIWE LA MSINGI KUZINDUA RASMI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli leo anatarajia kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya kisasa (Standard Gauge) katika eneo la Pugu Jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alipotembelea eneo la mradi huo lililopo Pugu Jijini Dar es salaam, amesema kuwa mradi huo utazalisha ajira nyingi katika kada mbalimbali.
Aidha, ameongeza kuwa mradi huo utakapo kamilika utarahisisha usafiri wa kutoka Dar es salaam hadi katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Mwanza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa kuwa safari ya Dar es salaam hadi Morogoro itatumia muda wa saa 1:16, huku Dar es salaam hadi Dodoma itatumia masaa 2:30 na safari ya Dar es salaam hadi Mwanza itatumia masaa 7:30.


Mradi huo ambao uko chini ya Kampuni za Merkezi ya Uturuki na Mota-Engil Afrika ya Ureno, kwa awamu ya kwanza utaanza na kipande cha kilomita 300 kati ya Dar es salaam hadi Morogoro kwa gharama zaidi dola bilioni moja za Marekani.
Source: Dar24

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search