TISA WAHOFIWA KUZAMA BAHARINI ZANZIBAR

Takriban watu 9 wanahofiwa kufa maji visiwani ZanzibarHaki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionTakriban watu 9 wanahofiwa kufa maji visiwani Zanzibar
Watu 9 hawajulikani waliko huku 44 waliokolewa baada ya mashua yao ya uvuvi kuzama nje ya pwani ya kisiwa cha Zanzibar.
Makarani Mohamed, ambaye ni kaimu mkurugenzi ya kitengo cha ujajususi aliambi BBC kuwa shughuli ya kutafuta na kuwaokoa watu bado inaendelea.
"Tunafahamu, kuwa ajali hiyo ilisababishwa na upepo na mawimbi makali yaliyosababisha mashua hiyo kuzama.Alisema.
Manusura mmoja waliwaambia waokoaji kuwa takriban watu 53 waliondoka kuenda kuvua samaki jana jioni wakati bahari ilikuwa tulivu.
Lakiki hali ya hewa ilibadilika na kusababisha mawimbi makali ya bahari.
Alisema kuwa hajawaona wenzake tangu ajali hiyo itokee.
Uvuvi ni shughuli kubwa ya kiuchumi katika kisiwa cha Zanzibar lakina mashua nyingi huwa zimechakaa hali ambayo husababisha ajali nyingi.
Manusura mmoja waliwaambia waokoaji kuwa takriban watu 53 waliondoka kuenda kuvua samaki jana jioni wakati bahari ilikuwa tulivu.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionManusura mmoja waliwaambia waokoaji kuwa takriban watu 53 waliondoka kuenda kuvua samaki jana jioni wakati bahari ilikuwa tulivu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search