UCHAMBUZI KISPOTI: SIMBA SC KABLA YA KUWACHEKA YANGA SC KUMBUKENI HAYA !!



Wakati gazeti la Mwanaspoti lilipoandika juu ya kutelekezwa kwa uwanja Bunju ulionunuliwa na viongozi wa Simba SC waliotangulia takribani miaka miwili au mitatu nyuma ; klabu husika na wanachama wake waliamka usingizini .

Waliamka usingizi kwa kwa kuandaa harambee ya kwenda kufyeka , kung'oa visiki na kutambua mipaka yake ili usije vamiwa na wajenzi holela .

Lilikuwa jambo jema na la kujivunia na hakika kila mwanamsimbazi alitoa kongole kwa uongozi na gazeti la Mwanaspoti.

Juhudi hazikuishia hapo , michango mbalimbali ilifanyika ili kasi ya ujenzi wa uwanja huo kufanyika . Nakumbuka tawi jipya la Wazo lilitoa ahadi ya kutoa mifuko ya saruji tani 1.5 na kundi la FoS matofali 10000!. Ili mradi kila mwanachama alionesha mwamko katika hilo kwa nafasi yake .

Lazima tukumbushane haya ...

Nyasi asili zilioteshwa ma mahasimu wao Yanga SC wakaanza kuingia hofu ya kupigwa gape la maendeleo na hapo kila uchao wakaanza kuusumbua uongozi.

Simba hawakuishia katika hatua za awali za ujenzi bali pia kuingia mkataba na kampuni fulani katika uuzwaji wa bidhaa zake hususani jezi na madukwa yakasambazwa jijini .

Kwa mbali binafsi nilianza kuona kauli mbiu yao ya ' NGUVU MOJA ' au ile mbadala ya ' TAIFA KUBWA ' inaanza kutimia .

Lakini klabu nzima kwa ujumla wake ilipoingia msimu wa 2016-17 vipaumbele vikabadilika . Ganzi ya kukosa ubingwa wa ligi kuu toka mwaka 2012 ikawaingia na kutelekeza ufanisu wa kila kitu na dira kuu ikageuka ubingwa.

Hamasa ya michango ikapotea na Bunju kutelekezwa . Mambo yakageuka si nyasi original bali bandia na zenyewe zikakwamia bandarini .

Matofali ya FoS na Saruji za Wazo zimegeuka hadithi . Mradi wa jezi na mapato mengine yakashindwa hata kulipia kodi nyasi bandia bandarini .

Hatamu ikawa kwenye viapo vya ubingwa na kuacha mambo ya msingi ambayo yanasimama kama vielelezo vya maendeleo klabuni .

Ujio wa MO ndio ukatandika jamvi la kudekea na kusahau kabisa rasimali watu kuijenga Simba mpya na Bunju yake .

Natizama kwa kina jinsi gani mnavyotumia nguvu kuwacheka wenzenu ambao wameuchukua ule mfumo ambao nyinyi mmeutupa ma kuanza kuijenga klabu yao upya . Mfumo wa Yanga kukusanya mapato kupitia wanachama wake laiti mngeuendeleza hakika leo Bunju Complex ingekuwa hadithi nyingine ya kuvutia na tambo jipya kwa watani zenu .

Simba na Yanga mmekuwa mkichekana kwa vitu vya msingi na mwisho wa siku wote mnadumaa katika umasikini na ujinga .

Leo nyinyi ambao mmeanza zaidi ya miaka miwili sasa kusimamia mauzo ya jezi zenu mnaweza kusimama mbele za watu na kusema hii ndio faida imetokana na mauzo ya jezi ?

Watani zenu wameamua kuinuka katika njia ambayo nyie mmeichepuka kama watafanikiwa katika hili watawacheka sana labda MO aichukue timu ndani ya muda mfupi ujao .

Kwa tetesi tu ndani ya saa 24 toka kuanzishwa kwa mfumo huu , Yanga imevuna si chini ya milioni 10 ! toka kwa wanachama wake wandamizi na dalili zinaonesha wanaweza kukusanya bilioni 3 ! kwa mwezi . Sasa endeleeni kuwacheka mwisho wa siku mtawapigia makofi .

IMEANDIKWA NA Samuel Samuel

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search