DUA YA SHEIKH #ALHADI #MUSA KWA ALIEKUA ‘BOSS WA FREEMASON’ SIR #ANDY #CHANDE IMEENDELEA KUZUA HISIA TOFAUTI MIONGONI MWA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU NCHINI.

Kufuatia Sheikh Mkuu wa Dar es salaam, kusoma dua maalum ya
kumwombea marehemu Andy Chande (pichani) ambaye ni mwenyekiti wa freemason
Afrika Mashariki. aliyeaminika kuwa na
imani kinzani wiki iliyopita imezua maswali miongoni mwa waumini wa dini ya
kiislamu.
Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alisoma dua hiyo maalum
ya kuwakumbuka waasisi wa shule hiyo na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akimbo
Rais Msaatafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa sanjari na wanafunzi
wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo.
Sir Andy Chande alifariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nchini
Kenyaalikokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa katika Makaburi ya Baniani,
Makumbusho jijini hapa kwa kuchomwa moto.
Katika enzi za uhai wake, Sir Andy Chande aliwahi kuweka
wazi kuwa yeye ni mfuasi na kuhani mkuu wa Jumuiya ya Freemason, jumuiya ambayo
inaaminika na baadhi ya watu kwamba iko kinyume na mafundisho ya dini za
Kiislamu na Kikristo. Katika tukio hilo la kuwakumbuka waasisi wa shule hiyo,
Shehe Alhadi aliongoza dua maalumu kwa upande wa dini ya Kiislamu kwa ajili ya
kumwombea marehemu Chande jambo lililoibua mjadala mkubwa.
Baadhi ya watu walihoji kuwepo kwa shehe mkuu wa Dar kwenye
dua hiyo wakati marehemu alijulikana kuwa ni Freemason ambayo wengi hawaiamini
kama ina sera za Mungu. Msikie huyu:
“Mimi binafsi sidhani kama ni sahihi kumfanyia dua mtu
ambaye aliwahi kuweka wazi kwamba yeye yupo upande wa kushoto, tena akiwa
mwenyekiti na kuhani mkuu wa jumuiya ambayo inaaminika inakwenda kinyume na
maadili ya Kimungu,” alisema Kimashi John kupitia ukurasa wake Facebook.
Mbali na Kimashi mijadala mingi iliyotawala mitandaoni siku
ya tukio hilo ilikuwa ni uwepo na uwakilishi upande wa dini ya kiislamu wa sheikh
Alhadi katika hafla hiyo
Gazeti moja maarufu kwa maswala ya udaku (Uwazi) baada ya
kuyasikia hayo, liliamua kumtafuta Shehe Alhadi mwenyewe ili kutoa ufafanuzi
juu ya suala hilo.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Shehe Alhadi
alikuwa na haya ya kusema:
“Katika dua niliyoiomba siku ile hakuna neno nililosema
kwamba Mungu aiweke roho ya marehemu Chande mahali pema peponi. Unaweza
kusikiliza tena rekodi za ile dua, nilichokifanya ni kumwombea kwa Mwenyezi
Mungu amlipe kwa mambo yote aliyoyafanya duniani maana yeye ndiye hakimu wa
mwisho.”
Aidha, katika hatua nyingine Uwazi lilipotaka kujua kama
alishawahi kumpa elimu ya dini ya Kiislamu, marehemu Sir Chande ikiwa ni pamoja
na kumtaka asilimu, Shehe Alhadi hakuwa tayari kulizungumzia hilo zaidi ya
kukiri kwamba amekuwa akifahamiana na marehemu kwa muda mrefu.
credit:blessnewstz




No comments:
Post a Comment