USALAMA MWANZA: #CHINA YAZINDUA MANUARI YA KWANZA YA KUBEBEA NDEGE ZA KIJESHI!

_63092241_a756ef43-d4e2-4c7c-896d-6835a5a7231f.jpg 

China imetangaza kwamba imefanikiwa kuzindua manowari yake ya kwanza ya kujiundia yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.

Meli hiyo ya kivita ina uzani wa tani 50,000.

Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.

Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.

Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.

Meli pekee kubwa ya kubeba ndege inayomilikiwa na China ni meli ya Liaonong, ambayo ni meli ya enzi za muungano wa Usovieti iliyofanyiwa ukarabati.

China ilinunua meli hiyo kutoka kwa Ukraine.

Chanzo: BBC Swahili

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search