#VYETI FEKI KUONDOKA NA 10,000; RAIS ATOA HADI TAREHE 15/5/2017 WAWE WAMEJIONDOA WENYEWE!


Rais Magufuli wa Tanzania amewafuta kazi wafanyikazi 10,000 wa serikali kwa kuwa na vyeti bandia vya elimu.
Amewaagiza kuwacha kazi ifikiapo Mey 15 la sivyo wakamatwe na kushtakiwa.
Hatua hiyo inajiri baa wafanyikazi hao kupatikana na vyeti bandia vya shule.
Kulingana na ripoti iliopokewa na rais Magufuli, takriban wafanyikazi 10,000 wa serikali wana vyeti ghushi vya shule.
Maelezo hayo yaliotolewa katika mji mkuu wa Dodoma yanaonyesha wafanyikazi 9,932 wa serikali walipatikana na vyeti bandia vya shule ya upili
Mwandishi wa wa taarifa hii  anasema kuwa hiyo ni asilimia 2 ya wafanyikazi wote wa serikali wapatao 435,000.
Akizungumza baada ya kupata ripoti hiyo, rais Magufuli amewapatia maafisa walio na vyeti hivyo wiki chache za kujiuzulu la sivyo washitakiwe.
Pia ameyataka magazeti nchini humo kuchapisha majina ya maafisa hao
Source:bbc Swahili 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search