Zuma 'acharuka' amfukuza kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan!

Kwa siku za hivi karibuni Zuma amekuwa na ushawishi mdogo ndani na nje ya chama cha ANC
Image captionKwa siku za hivi karibuni Zuma amekuwa na ushawishi mdogo ndani na nje ya chama cha ANC
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko haya.
Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.

Takriban maafisa 15 wametimuliwa katika kile kinachotajwa kama mshangao kwa serikali ya Zuma.

Aliyekuwa waziri wa fedha Pravin Gordhan
Image captionAliyekuwa waziri wa fedha Pravin Gordhan
Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani.
Maafisa kadhaa kutoka chama tawala cha ANC wanapinga kuondolewa kwa Gordhan

Source: BBC swahili news.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search