#ZUWIWO: POLISI WASEMA TUKIO LA KUFANYA USAFI CUF (HQ) NI HATARISHI; WATAKA USAFI UANZE KATIKA NGAZI YA FAMILIA!

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kitendo cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka maeneo mbalimbali kwa kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani atakethubutu kujitokeza atachukuliwa hatua za kisheria leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionesha madumu ya pombe haramu ya Gongo yaliyo kamatwa katika oparesheni ya jeshi la polisi leo jijini Dar es Salaam.
Picha za magari yanayodaiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu jamii.

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imezuia wanachama wa CUF kufanya usafi katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni kutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani kutokana mvutano wa makundi mawili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema ombi la kufanya usafi katika mazingira ya ofisi za chama hicho, lililowasilishwa na Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea Aprili 27 mjini Dodoma.

Amesema kutokana na sababu za kiusalama pamoja na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea ndani ya chama hicho, Mbunge huyo pamoja na wanachama wengine na wanashauriwa kila mmoja kufanya usafi katika eneo lake analoishi au analofanyia kazi.

"Kitendo hicho cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka katika maeneo mbalimbali kwa kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani na atakayethubutu kujitokeza atachukuliwa hatua za kisheria," amesema Sirro.

Wakati huo huo Kamanda Sirro amesema sakata la watu waliovamia mkutano wa iongozi wa CUF wilaya ya Kinondoni na wanahabari hadi sasa wanawashikilia watu saba akiwemo Mkurugenzi wa Mahusiano wa wa chama hicho, Abdul Kambaya.

Amesema upelelezi wa kesi hiyo, umefanyika vizuri na tayari jalada limefikishwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Jeshi hilo pia limewataka wananchi waliowahi kuibiwa magari yao kujitokeza katika Kituo cha Polisi Mbezi ili kuangalia kutokana,na kupatikana kwa magari matano yanayodaiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.

credit: Globu jamii

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search