Countdown!! Siku mbili kabla ya Harusi yake Flora Mbasha asema "nilitamani mume atakaenijali na kuniheshimu"

“Sing-bird” wa musiki wa injili maarufu kwa
jina Flora Mbasha, amefunguka mambo kadhaa siku chache kabla ya ndoa yake mpya
inayotarajiwa hivi karibuni.
![]() |
Mwanadada Flora katika ubora wake ! |
Flora(pichani juu), ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa muhubiri maarufu nchini, Askofu,
Moses Kulola (sasa marehemu), katika mahojiano aliyofanyiwa na mtangazajia wa
Tv moja ya burudani hivi karibuni, Flora amesema ilikuwa ndoto yake kupata mume
bora, atakaemuheshimu na kumjali kama mke.
Kwa sasa maandalizi ya harusi yanaendelea na tayari ameshabadilisha jina
lake la kisanii akitaka mashabiki wake wamtambue kama “Madame Flora” badala ya
jina lililozoeleka la Flora Mbasha.
No comments:
Post a Comment