#Asha Ally Mabula: 'Macho kwako Miss Super Model 2017'

Mtanzania Miss Asha Ally Mabula amekabidhiwa rasmi Bendera ya Tanzania tayari kwenda Kuiwakilisha Nchi katika mashindano makubwa ya Miss Supper Model 2017 yanayofanyika Mjini Macau, China.

Akizungumza katika hafla maalum ya kukabidhi bendera, Mgurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Bibi Leah Kihimbi alimtaka Asha kujituma katika mashindano hayo ili kuiletea Tanzania ushindi na kuipaisha Kimataifa.


Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akizungumza wakati wa tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarjia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo.
A
 Miss Super Model 2017 Asha Ally Mabula akizungumza wakati wa tukio la kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Word Super Model 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo. Kutoka kulia ni Afisa Utumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi na Meneja Mkuu wa Tanzania Miss Super Model Ibrahim Thabit.
A 1
Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akimkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo. Katikati ni Afisa Utumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
A 3
Baahi ya waandishi wa habari wakishuhudia tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa Miss Word Super Model, Asha Ally Mabula anayetarajia kushiriki mashindano hayo Macau nchini China.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search