Benki Ya NMB Yazinduwa ‘Fanikiwa Account’ Kwa Wafanyabiashara Wadogo



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron akifafanua jambo katika uzinduzi wa ‘NMB FANIKIWA ACCOUNT’. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard (kushoto).

BENKI ya NMB imezindua akaunti mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ijulikanayo kama ‘NMB FANIKIWA ACCOUNT’ ili waweze kukua kibiashara pamoja na kupata maendeleo ya biashara wanazozifanya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa akaunti hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo haina masharti magumu wakati wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake hivyo kuwataka wafanyabiashara wote kuitumia.
Alisema kuwa NMB imebuni akaunti hiyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya wafanyabiashara wadogo kukosa mikopo na kukabiliwa na riba kubwa kwenye mikopo. Akifafanua zaidi juu ya bidhaa hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara, James Meitaron alisema Benki ya NMB imeweza kufikia kila kundi katika kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo hasa kimikopo ambapo imewanufaisha katika kuendeleza biashara zao.
Alisema Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na taasisi zake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inawakuza wafanyabiashara wadogo na wakati wakiwemo ‘mama lishe’.

Mkutano huo ukiendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa Benki ya NMB kushoto.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search