Yametimia... "Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo Out'

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, Mchana huu ametengua rasmi Uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Pro. Muhongo.



Utenguzi huo umekuja masaa kadhaa baada ya ya Rais Magufuli kumuambia Prof. Muhongo ajipime mwenyewe kama anatosha kuendelea kuwa Waziri wa Wizara hiyo kutokana na utata uliojitokeza wa waziwazi wakati wa Uwasilishaji wa Ripoti Maalum ya Kamati iliyoundwa na Rais kuchunguza Makontena ya Mchange wa Madini.

Ripoti hiyp imemuhusisha yeye kama Waziri mwenye dhamana kushindwa kuishauri Serikali na kuisababishia nchi hasara kubwa !

Tumekuwekea taarifa rasmi tuliyoipokea mchana huu kwa hisani ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search