BREAKING NEWS!! Philemon Ndesamburo aaga Dunia, #SHARE ..Mwanawe Mhe. Lucy Owenya akubwa na Taharuki !
Tumepokea habari ya kusikitisha ya kifo cha ghafla cha Mwanansiasa Mkongwe hususan kwenye Anga za Siasa za Upinzani Nchini' Bwana Philemon Ndesamburo.
Mtoto wa Marehemu Mbunge wa Viti Maalum Maalum Mkoa Kilimanjaro Mhe. Lucy Owenya(Pichani chini), aliekuwa Bungeni Mjini Dodoma akihudhuria vikao vya Bunge la Bajeti, alikumbwa na mshtuko mkubwa baada ya kupokea Taarifa hizo.
Kwa mujibu ya maelezo yanayotembea mtandaoni na ambayo Matukio Blog inayafanyia kazi, Mzee Ndesamburo amefariki mara baada ya kufikishwa hospitalini kufuatia kupoteza nguvu ghafla alipokuwa 'akisaini cheki' kwa ajili ya mchango wa Rambirambi kwa wafiwa waliopoteza wapendwa wao kwenye ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.
Mzee Ndesa au 'Ndesa Pesa' kama mashabiki wake walivyopenda kumuita, alizaliwa Mwaka 1935, na amewatumikia wananchi wa Moshi Mjini kwa kuanzia mwaka 2000 mpaka alipoamua kustaafu rasmi nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA.
#Matukio Blog inaungana kuwapa pole wafiwa na kumuombea Marehemu Ndesamburo !
No comments:
Post a Comment