Dunia Kwishaa, kwisha kabisa.. #SHARE: Wanawake waandamana kudai haki ya kubaki vifua wazi kama wanaume !
Hebu Soma hii uone ulimwengu unakoelekea sasa.. Ni Hatari aisee..
Kuna dhehebu la watu wanajiita Waraelian.. pamoja na madai
mengine kundi hili linapigania haki ya ‘mwanamke
kuvaa sawa na mwananume ikiwemo kuachia sehemu kubwa ya kiwiliwili chao wazi kama
wanavyofanya wanaume..
Katika kuhakikisha lengo lao linatimia, kundi hili limekuwa
likipigia debe siku ya Aug. 24 kila mwaka iwe ni siku maalum ya wanawake kubaki
vifua wazi na wamewaomba wanaume duniani kote 'kuwasapoti' kwa kujichanganya nao
bila kuvaa nguo maeneo ya juu ya kiuno hadi kifuani.
Msemaji wa kundi hilo la harakati kutoka Marekani,
alivyoulizwa endapo kwa kitendo hicho hakitamtia mwanamke kwenye fedheha
alijibu hapana.. "hatuwezi kuona aibu wala fedheha, tunataka kudumisha mapenzi binafsi
na upendo kwa kila mmoja wetu…" alimaliza msemaji huyo aliejulikana kwa jina la Bi Rachel ambae ni mwananchama wa kundi la UFO lililoandaa maandamano ya mwaka huu…
MatukioTZA imeshindwa kukuwekea picha zote kwa sababu za
kimaadili, tumeweka chache tu ingawa kwa shingo upande!!
#share
#share
No comments:
Post a Comment