Exclusive News! Trump asalimu amri, sasa yuko Tayari kukutana na hasimu wake mkuu kiongozi wa korea Kaskazini.



Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kukutana uso kwa uso na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un endapo atapata nafasi ya kufanya hivyo.
Akijibu swali katika mahojiano maalum na jarida maarufu la Bloomberg jana tarehe 1 May, Trump alisisiza bado ni ndoto yake kubwa kukutana na kiongozi huyo mtata wa N. Korea.. “Kweli nisingesita kufanya hivyo, tena hilo ni jambo la heshima kubwa kwangu”
Kauli hiyo ya Trump imeonekana kama hatua ya ‘kulamba matapishi yake’ imekuja wakati hali ya sintofahamu ikizidi kutamalaki kufuatia Marekani na washirika wake kujiandaa kufanya majaribio kadhaa ya silaha za kiatomiki kujibu majaribio kama hayo yaliyofanywa na Pyongyang.

 “Mwanasiasa shujaa kabisa angelipa mgongo ombi la kukutana na kiongozi huyo mtata zaidi wa Korea Kaskazini lakini kwangu mimi ni jambo ninalolisubiri kwa hamu na shauku kubwa” alimaliza Bw. Trump.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search