Kutoka Bungeni: Ona hapa Wabunge walivyopaza sauti kumnasua Halima Mdee kifungoni !
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenister Mhagama amependekeza kufanyika kwa mabadiliko ya hoja na kupendekeza Mhe. Mdee asamehewe... hata hivyo ametoa tahadhari endapo atatenda kosa jengine la kudharau mamlaka ya Bunge utekelezaji wa adhabu uanze mara moja bila kuitisha kikao cha kamati ya maadili.
Kupitia vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea Makao Makuu Dodoma, leo Jumanne Wabunge wa pande zote bila kujali itikadi za vyama vyao, wamemwomba Spika kutoa msamaha kwa Mbunge Halima Mdee aliyepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobakia.
Baada ya Wabunge kwa umoja wao kuomba kiti cha Spika kutompa adhabu hiyo Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Bunge limetangaza kumsamehe na ataendelea na vikao kwa sharti la kutorudia tena kosa.




No comments:
Post a Comment