Mo Dewji 'awazodoa Simba' asema Wadhamini wenye 'Mikwanja' zaidi ya SportPesa wapo!!!

Mo Dewji- Mfadhili wa klabu ya Simba na Tajiri mtoto kuliko wote Barani Africa kwa Takwimu za Forbes!
Mfanyabiasha maarufu Nchini Tanzania na Mfadhili wa mda mrefu wa Klabu ya Simba 'wa Kimataifa' watoto wa Msimbazi jijini Dar es Salaam Mo Dewji amelaani vikali kitendo cha viongozi wa Simba kuingia makubaliano ya Ufadhili bila yamashauriano.

Akitoa kauli kali kupitia ukurasa wake wa 'twitter', Mo ambae pia alikuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Singida kwa mda mrefu, aliwalaumu viongozi hao na kwamba hakukuwa na uharaka wa kufunya kwani kuna wadhamini wenye mkwanja mnene zaidi ya huu walioukimbia wa SportPesa..
" nimelipa mishahara miezi 8 zaidi ya milioni 750 na nimesaidia usajili wa dirisha dogo ndani ya Simba SC . Wamenipigia simu jumatano kwamba wamepata mdhamini nikawaambia tukutane weekend tulijadili maana hapo nyuma tulipata mdhamini ambaye yupo radhi kutoa bilioni 2 kwa mwaka na wanajua hilo ... tulikuwa tunasubiri muda tu tuingie mkataba sasa imekuwaje ghafla waingie mkataba wakati hatujaongea na makubaliano yapo ?! ..." alimaliza Mo ambae pia ndie Tajiri mtoto kuliko wate barani Africa kwa mujibu wa Jarida la Forbes..

endelea kufuatilia blog yako ya matukio: www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com

ciaoo..

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search