Habari za Hivi Punde! Kuna Taarifa ya ufyatuaji Risasi Maeneo Ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam kati ya Polisi na Ndugu Adam Malima aliekuwa Mbunge wa Mkuranga!!

Bw. Adam Malima katika moja ya matukio wakati alipokuwa akitumikia moja ya Nyadhifa - Serikalini.
Kuna Taarifa ya ufayatuaji Risasi hewani wakati wa tukio lililomuhusisha Mbunge wa zamani Wa Mkuranga Ndugu Adam Malima.



Kwa mujibu wa 'Video clip' iliyosambaa machana huu kupitia mitandao ya kijamii inaonyesha askari waliovalia sare za Jeshi la Polisi na Mbunge huyo wa zamani ambae pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini ikiwepo ya Unaibu Waziri wa Fedha chini ya Awamu ya Dk. Jakaya Kikwete wakirushiana maneno makali kabla milio ya risasi kusikika huku Bwana Malima nae akijibu vikali majibizano hayo ya maneno baada ya kutoka kwenye gari lake kukabiliana na 'valangati hilo' !!

endelea kutega masikio nasi tukiendelea kufuatilia habari hii kwa kina kupitia:
www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search