Jokate apeleka ombi kwa wadau kutatua changamoto !

Miss Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa  Umoja wa Vijana  wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao.

A 1
Miss Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa  Umoja wa Vijana  wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi cheti  kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao.
A 2
Kaimu Mkuu wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa akizungumza katika mahafali hayo
A 3
Jokate Mwegelo akizungumza katika mahafali hayo
A 4
Dada Mkuu wa shule ya Jangwani akimrisha keki Jokate katika mahafali hayo
………………………………
Na Mwandishi wetu
Mwanamitindo, muigizaji  na Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo ametoa wito kwa watu maarufu nchini kusaidia kuondoa changamotokatika sekta mbalimbali ili kupunguza mzigo  serikali.
Jokate alisema hayo wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani ambapo jumla ya wanafunzi 118 walimaliza shule.
Mrembo huyo ambaye ni Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa  Umoja wa Vijana  wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) amesema kuwa Tanzania ina watu wengi maarufu na wenye uwezo, lakini wachache tu ndiyo wamekuwa wakijitolea kusaidia sekta mbalimbali husasani elimu na afya.
Alisema kuwa kwa hali ilivyosasa,ni vigumu kwa serikali kutatua matatizo yote na kuwaomba  wanamuziki, wasanii, wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali kujitolea kusaidia kutatua matatizo katika jamii.
Alifafanua kuwa shule ya wasichana ya Jangwani ni kongwe  kutokana na kuanzishwa Mei 28, 1928, lakini mpaka sasa inakabiliwa na matatizo mbalimbali wakati kuna wahitimu wengi ambao kwa sasa wana nyandhifa na wanashindwa kuchangia.
“Mimi sijasoma Jangwani, lakini niliguswa na matatizo ya viwanja vya michezo na kuamua kujenga uwanja wa mpira wa kikapu na mpira wa pete (netiboli), nashukuru viwanja kwa sasa vinatumiwa na shule zinazozunguka maeneo haya,naomba wengine wasaidie, kuondoa changamoto zilizopo,” alisema Jokate.
Mrembo huyo pia amewaomba viongozi wa serikali na wafanyabiashara  waliosoma katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Jangwani, kusaidia kuondoa changamoto za shule hiyo.
Awali, Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Amos Mgongolwa alisema mbali ya uchakavu wa majengo, shule yao haina madarasa na mabweni ya kutosha, haina  ukumbi wa kufanyia shughuli mbalimbali kama sherehe na kulazimika kufanyia eneo la wazi, shule haina hata gari moja kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na matibabu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mgongolwa amesema wanafunzi wenye mahitaji maalum, ulazimika kutumia baiskeli za miguu mitatu ili kwenda  kwenye shughuli mbalimbali za kimamoso nje ya shule.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search