Kikanda na Kimataifa: Stella Nyanzi arudishwa gerezani Uganda

 Mahakama KUU nchini Uganda imemrejesha gerezani msomi na mkosoaji mkubwa wa Rais Yoweri Museveni bibi Stella Nyanzi. 


Mahakama Kuu nchini Uganda imemrudisha gerezani msomi na mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni na kufunguwa njia ya kufanyiwa uchunguzi wa akili wa lazima.
Stella Nyanzi mhadhiri na mtafiti wa chuo kikuu ametiwa gerezani zaidi ya wiki mbili zilizopita wakati nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilipomfungulia mashtaka kuhusiana na makosa ya mtandaoni.Makosa hayo yanatokana taarifa alizoweka kwenye mtandao wake mashuhuri wa facebook ambapo amewashutumu Museveni na mke wake kwa kuvunja ahadi ya uchaguzi ya kutowa vitaulo vya wanawake vya kujistiri wakati wa kupata siku zao.
Mke wa Museveni ni waziri wa elimu nchini Uganda. Msomi  huyo alikuwa amefikishwa mahakama kuu kuomba dhamana baada mahakama moja ya chini kukataa kusikiliza kesi hiyo. Pia alikuwa akitaka mahakama hiyo kuu kuacha kuzingatia ombi la serikali la kutaka afanyiwe uchunguzi wa akili.
-DW 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search