Mbunge wa Moshi na Meya wake Raymond Mboya wakwama kumuona Rais;

Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael na Meya wa Mji huo, Raymond Mboya (Chadema), walijikuta wakiishia getini katika Ikulu ndogo mkoani kilimanjaro mara baada ya kuzuiliwa kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili mkoani humo.

Aidha, kwa mujibu wa mtandao wa Dar24, hatua hiyo ilifikiwa mara baada ya kutokuwepo kwa taarifa zao kuhusu kuonana na Rais Dkt. John Magufuli.
“Ni kweli niliondolewa kwenye foleni, alikuja Ofisa usalama mmoja akaniambia kistaarabu kuwa mimi sikuwa nahitajika katika kikao hicho, nilijaribu kumwambia kuwa mimi ni mbunge lakini akasisitiza kuwa sihitajiki,”amesema Michael.
Kwa upande wake Meya wa Moshi Mjini, Raymond Mboya amesema kuwa alipewa taarifa na viongozi wa Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwa wanahitajika katika kikao hicho cha Rais Dkt. Magufuli ambacho kilipangwa kwaajili ya kukutana na viongozi wa dini.


Hata hivyo, Rais Dkt. John Magufuli yuko Mkoani Kilimanjaro kwa ajili maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search